Posted:Wed, 26 Jun 2013 16:54:00 +0000
Kombati za CHADEMA mzozo
Siku
moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe na wabunge wenzake watatu kuzuiwa kuingia bungeni juzi, uongozi wa
Bunge umesisitiza kuwa kombati zao zinakiuka kanuni.
Mbowe na
wabunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless
Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari
kwa madai kuwa wamevalia sare za chama ambazo kikanuni haziruhusiwi.
Uamuzi
huo uliibua hali ya sintofahamu kwa wabunge wa CHADEMA kutokana na
Mbowe kuvalia vazi hilo mara nyingi tangu aingie bungeni mwaka 2010.
Licha
ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la ‘safari suti’ kwa wanaume lenye
mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA,
Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa uamuzi huo unaacha maswali mengi
yanayohitaji majibu.
Akizungumzia uamuzi huo jana, Mkurugenzi wa
Shughuli za Bunge, John Joel alisema suti hizo za wabunge wa CHADEMA
zilikiuka kanuni ya 149 (3) (b) (i).
Kipengele hicho cha kanuni
kinasomeka kuwa inaruhusiwa suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu
au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila
fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila
baragashia.
Joel alifafanua kuwa yawezekana huko nyuma wamekuwa
wakifanya makosa kwa kuwaruhusu wabunge hao kuingia na suti hizo,
lakini sasa kuanzia juzi wameamua kuanza
kuchukua hatua ya kuwazuia.
“Zile
wanasema sio sare ya chama, lakini wote tunawaona kwenye mikutano na
shughuli za chama ndizo zinavaliwa na isitoshe tuliwahi
kuwatahadharisha kuwa ziko kinyume na kanuni wasizivalie bungeni ila
wamekuwa wakiendelea kuzivaa,” alisema.
Licha ya kanuni hiyo kuwa
kimya kuhusu kuvaa sare za vyama bungeni, Joel alisema kuwa uamuzi huo
ulikuwa ni busara ya spika wa wakati huo, Samuel Sitta, lakini
haujaingizwa kwenye kanuni kimaandishi.
Tanzania Daima Jumatano
lilitaka kufahamu ni kwanini uamuzi huo ukaanza ghafla juzi baada ya
wabunge wa CHADEMA kurejea kutoka jijini Arusha, na Joel bila kufafanua
alisema: “Kawaulize walipanga nini wakiwa Arusha? Ndiyo maana tukaamua
kuchukua hatua.
“Bora tukaonekana tumewaonea kuliko kuendelea
kufumbia macho kanuni. Tuwe wawazi kombati zao zina nakshi kupitiliza
kwa mujibu wa kanuni. Kwanini wakina Halima Mdee na Vicent Nyerere
tuliwaacha wakaingia? Mbona kombati za Zitto zinatofautiana na
wengine?”
Alipotakiwa kufafanua kama kweli walishaonywa wasivae kombati hizo bungeni,
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Habari wa CHADEMA, John Mnyika alisema Joel hajui
kanuni za Bunge ndiyo maana amekuwa anampotosha spika na viongozi wa
Bunge kufanya uamuzi wa ajabu.
“Wametuzuia juzi kwa sababu ya
maelezo ya akina Pinda na Serikali ya CCM, sio kwa sababu ya ukiukwaji
wa kanuni za Bunge. Kumekuwa na utamaduni wa hovyo wa kutafsiri vibaya
kanuni za Bunge kwa lengo moja tu, kuwadhibiti CHADEMA,” alisema.
Mnyika
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alitolea mfano akisema kuwa
walizuiliwa kuingia ukumbini na askari polisi wasiokuwa na mamlaka ya
kuwazuia kuingia ndani bali walitakiwa wasubiri amri ya spika kuwatoa
ukumbini ndipo wawatoe.
“Hayo yote hawezi Joel kufahamu,
anafanyia uzoefu alioupata wakati anafanya kazi Makao Makuu ya CCM
wakati wa Bunge la chama kimoja,” alisema Mnyika.
Akizungumza na
waandishi wa habari juzi, Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa kambi ya
upinzani bungeni, alisema kuwa walishangazwa na uamuzi huo wakati
mavazi hayo wamekuwa wakiyavaa miaka yote na kuingia nayo bungeni.
Lissu
alisema kuwa hatua hiyo waliichukulia kama mkakati maalumu wa Serikali
ya CCM kutaka kuwazima kabisa kuhakikisha hawapati nafasi ya kuingia
bungeni ili kujibu tuhuma walizosingiziwa kuhusiana na mlipuko wa bomu
jijini Arusha.
“Sisi hali hiyo tulianza kuishtukia tangu asubuhi
tulipoingia kwenye eneo la Bunge, kama mligundua kulikuwa na askari
wengi sana kila kona kuliko kawaida kana kwamba nchi imepinduliwa.
Kinyume na utaratibu wa kanuni askari wa kawaida wameingizwa hadi
bungeni,” alisema.
Hata hivyo, pamoja na uamuzi huo, kanuni za
Bunge hakuna mahali zinazuia mbunge kuvaa sare ya chama chake isipokuwa
kanuni zimeainisha aina za mavazi ya kuvaliwa na wabunge wanawake na
wanaume.
Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3)(b) kwa wanaume
wanaruhusiwa kuvaa (i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au
mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana
ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia;
(ii)
vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na
makubadhi au viatu; (iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadiri
isiyomeremeta; (iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote
ya heshima; au (v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba
chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.
TMBELEA gumzo la jii
http://talkbongo.blogspot.com/
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home